TENGENEZA, HIFADHI NAMNA HII MARISHO YA NG'OMBE...


JINSI YA KUHIFADHI MALISHO KWA NJIA YA HEI (HAY)

HAY ( majani makavu )

HEY ni namna ya kuhifadhi malisho ambapo majani hukatwa kutoka shambani,hukaushwa juani na kutunzwa sehemu maalumu kwa ajili ya kutumika wakati ujao.Mara nyingi mfumo huu hutumika kutunza malisho ili yaje kutumika wakati wa kiangazi ambapo malisho hupungua.

Wafugaji wengi nchini wamekuwa wakisumbuka sana hii ni kwa sababu ya kutokuwa na chakula Cha kutosha kwa mifugo Yao kwa mwaka mzima Hali inayopelekea kupungua kwa uzalishaji na pia hata kufa kwa mifugo kwa sababu ya njaa.Wafugaji wengi hutegemea malisho ya asili ambapo eneo moja hutumiwa na wafugaji wengi na kupelekea Uhaba wa malisho.

Hivyo basi wafugaji hawana budi kubadili mfumo wa uzalishaji malisho ambao utawafanya kufuga kisasa kwa kuwa na malisho binafsi kwa ajili ya mifugo Yao kitu ambacho kitafanya kuwepo kwa malisho ya kutosha kwa wafugaji ili kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi .

Kuvuna nyasi na kuzihifadhi kwa mfumo wa nyasi kavu ni bora zaidi kwa sababu huzuia upotevu wa chakula kwa kukanyagwa na kuchafuliwa hovyo na wanyama, badala yake mfugaji huweza kulisha kulingana na mahitaji.Hata hivyo kwa vile, hei ndio mfumo unaotumika zaidi kuhifadhi nyasi kwa ajili ya mifugo, mfugaji lazima atambue sababu zinazosababisha ubora wa hei pamoja na namna ya kutambua hali ya ubora wa hei aliyoitunza.

Ubora wa hey unasababishwa na;

•Aina ya nyasi.Nyasi hutofautiana kiwango cha virutubisho na madini kwa ajili ya mifugo. Pia vile vile uwezo wa kufyonza katika udongo na ukuaji wake.

Mfano wa aina ya malisho yanayofaa kwa kutengeneza hei ni majani boma (Rhodes grass), Lucerne (alfalfa),mahindi,mtama n.k

•Ukuaji wake.ubora wa hei hupotea haraka kadri nyasi zinavyozidi kukomaa. Hivyo mfugaji hushauriwa kuvuna nyasi mapema kabisa baada ya kuanza kutoa maua.

•Hali ya hewa na utunzaji wake.mfano baada ya kuvuna mvua ikinyeshea nyasi husababisha upotevu wa virutubisho. Pia vilevile jua kali husababisha upotevu wa Vitamini A na kupukutika (kuvunjika vunjika) kwa majani.

•Kiasi cha mbolea kwenye udongo.kiwango ch

a kutosha cha madini ya chokaa, nitrojeni, fosifeti (phosphate), Potassium (K) na madini mengine yanayohitajika kwa kiasi kidogo ni muhimu kwa ajili ya kuzalisha hei yenye ubora.

JINSI YA KUANDAA HEI BORA

1.kuvuna nyasi

Kata nyasi kwa mkono au mashine katika kipindi kinachotakiwa ,(appropriate growth stage)unashauriwa kukata nyasi kwa ajili ya kutengeneza hei kabla majani hayajaanza kutoa maua

2.kausha nyasi

Baada ya kukata nyasi zikaushe kwenye juakwa kuzitandaza chini kwa siku mbili au tatu kulingana na Hali ya hewa ya eneo husika .pia unaweza kuzisimamisha kwenye Mti ili kuruhusu kupotea kwa maji kwenye majani

3.kusanya nyasi

Zikusanye nyasi zako kutoka eneo ulipokuwa unazikausha .unaweza kukusanya nyasi kwa kubeba kwa mkono au kwa kutumia mashine maalumu .

4.kufunga nyasi

Nyasi hufungwa na kuhifadhiwa katika boksi maalumu kulingana na uzito (simple wooden baller) au kwa kutumia trekta au mashine maalumu na hata pia kwa kutumia mkono na kamba.Hii inarahisisha kusafirisha mizigo kama nyasi zinaenda eneo la mbali

5.kuhifadhi hey

Hifadhi hey kwa ajili ya malisho katika eneo kavu lisilozidi unyevu wa 20%.Hii itasaidia hey kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika

KUMBUKA

Kabla ya kulisha hei mifugo yako chunguza ubora wake kwa kuchunguza nje na ndani ya hei ulizozihifadhi kwa kuzitawanya ili kujiridhisha ubora wake.

Hey bora /zinazofaa Zina sifa zifuatazo

•zina majani mengi na zenye kijani

•zina harufu nzuri

•Zina matawi kidogo 

•Ni safi zisizo na uchafu wa aina yeyote

Hey zisizofaa kwa mifugo Zina sifa zifuatazo

•matawi mengi kuliko majani

•Harufu kama zimeoza

•Ni chafu

Post a Comment

Previous Post Next Post