NG'OMBE WA NYAMA NA MAZIWA, FAHAMU ZAIDI...

 


Katika ufugaji wa mifugo kuna vitu ambavyo unatakiwa kuvifahamu wewe kama mfugaji au mtu mwenye malengo ya kufuga.

Wanyama wamegawanyika katika makundi tofauti tofauti kulingana na asili zao lakini pia kazi zao ( purpose )

Kwa mfano; kuna kuku kwaajili ya nyama, kuna kuku kwaajili ya mayai, kuna ng'ombe kwaajili ya nyama, kuna ng'ombe kwaajili ya maziwa, kuna mbuzi kwaajili ya maziwa, kuna kondoo kwaajili ya kuzalisha manyoya yanayo tumika katika kutengeneza bidhaa mbali mbali kama vile nguo.

Sasa mtu unapo hitaji kufuga moja wapo ya wanyama tulio wataja hapo juu, yakupasa ujiulize maswali wakaza kuwa mfano; unataka kufuga ng'ombe, sawa lakini swali nikwamba utafuga ng'ombe wa aina gani na kwaajili ya nii ? yaani hapa utajiuliza kulingana na lengo kuu la wewe kuhitaji kufuga, kama soko lako linalenga kuuza nyama basi utafuga ng'ombe kwaajili ya nyama, kama unaona kabisa Sehemu niliyopo kuna uhitaji wa maziwa basi utafuga ng'ombe wa maziwa.

Hivyo hivyo na kwa mifugo wengine kama vile kuku, kama unaona mahali ulipo kuna uwezekano wa kuuza mayai basi utafuga kuku wa mayai. Pia kama unaona mahali ulipo kuna uhitaji wa nyama basi utafuga kuku wa nyama.

Kwahiyo ni muhimu sana kujua kitu gani utakiuza kutoka kwa hao mifugo una hitaji kuwafuga ikiwa umezingatia na mahitaji ya jamii inayo kuzunguka.

Huu ndiyo ufugaji wenye tija na sisi kama lugalo Animal Care Platform tupo kuku habari zinazo husiana na ufugaji wenye tija, karibu sana...

Post a Comment

Previous Post Next Post