MUHIMU KATIKA KUPOKEA VIFARANGA, KIENYEJI, KISASA NA CHOTARA...


 
SOMO KUHUSU VIFARANGA

Kwa Kifupi Sana fanya yafuatayo utanishukuru

Kwanza kabisa vifaranga wanahitaji Sana Mambo yafuatayo yazingatiwe.

1) Joto

2) Chakula Safi

3) Maji Safi

4) Mzunguko mzuri wa hewa

5) Idadi sahihi ya Vyombo vya chakula na Maji

6) Randa Safi ,zisizo na vumbi, kavu

KUMBUKA, utanufaika na mafunzo haya endapo utayafanyia kwa vitendo

WIKI LA KWANZA

Siku ya kwanza kabisa ( Glucose/Glucovet.. inategemea wametoka umbali gani wanaweza kupewa masaa 3-24).

 Multivitamins Mfano! Neoxychick, Chick formula ,Tetracovit Kwa siku ya kwanza Hadi ya 5 ( SIJAANDIKA DAWA HAPO).

Siku ya 6 huwa tunashauri wapewe maji tupu, 

Siku ya Saba ni chanjo ya kwanza ya NEWCASTLE/ KIDERI-MDOND

Muda huu wote watakua wanatumia chakula cha Starter/ Broiler starter.

WIKI LA PILI

Siku ya nane Hadi siku ya 12 Wapewe vitamins zipo Aina nyingi Sana Mfano :Aminototo, Farmvita, Dad OCTAVIT, Amylyte, Vitalyte n.k

Siku ya 13 wapewe maji matupu ( japo hata ukiwawekea vitamins si mbaya).

Siku ya 14 wapewe chanjo ya Pili ya Infections Bursal Disease / Gumboro

Muda huu wote wapewe chakula cha Starter/ Broiler Starter.

WIKI LA TATU

Hapa tuna wagawa kuku kutokana na Aina

KUKU WA NYAMA/BROILERS

Siku ya 14 au15 Hadi ya 22 wapewe Grower Pellets ( Kwa uzoefu wangu). 

Hapa hawa kuku wanaweza kupewa Broiler Booster Mfn : Utravin broiler booster.

Siku ya 21 kuku Broiler wapewe chanjo moja wapo Kati ya Gumboro au KIDERI ( Hii inategemea MAZOEA ya namna ya kuchanja kuku kutokana na mkoa ulipo). 

KWA KUKU WANAOANDALIWAKUTAGA ( CHOTARA, LAYERS , KUKU WA KIENYEJI).

Wapewe chakula cha Starter Mashi inaenda mpaka wiki ya 7 au wiki ya 8 (inategemea maelezo ya chakula unachotumia na kampuni uliyo nunua chakula).

Siku ya 21 kuku hawa watapewa Chanjo ya pili ya Newcastle/KIDERI/MDONDO

Siku ya 28 kuku wanao andaliwa kutaga wapewe chanjo ya pili ya Gumboro

Siku ya 30-35 ni chanjo ya Ndui (Japo maeneo mengine Ndui hutokea mapema wiki ya 3).

Kila baada ya miezi mitatu kukuwako wapewe chanjo ya KIDERI/ Newcastle

KUMBUKA

Minyoo ni hatari Sana Kwa maendeleo ya kuku....unapaswa kuwapa dawa za minyoo mapema Kwa mara ya kwanza wakifika miezi miwili , Kisha utakua unarudia kila baada ya miezi mitatu USIPUUZE

Kwa chakula wape grower mash wiki ya nane au 9 mpaka wiki ya 18-19 ( Pale utakapo okota yai bandani).

NB : Kuku hawa wapewe vitamins mara Kwa mara ..sio lazima kuwapa kilasiku kupunguza Gharama

Kuku wako wakifikisha asilimia 3-5 za utagaji wape Layers mash moja Kwa moja Hadi pale utakapo amua kuja kuwauza

Ikumbukwe kuku hawa wanapaswa Kula Kwa kipimo maalumu kutokana na Umri

MAZOEA YANAONESHA WATU KUFUGA KWA KUWEKA RATIBA YA DAWA KAMA CHAKULA

Hii sisawa Kitaalamu , kuku wapewe dawa pindi wanapoumwa...Uzoefu wangu haunioneshi ulazima wa kukuza kuku Kwa Dawa.

Post a Comment

Previous Post Next Post