LIJUE HILI KABLA HAUJAKATA TAMAA KUFUGA KUKU...

 


 MAWIO NA MACHWEO KATIKA UFUGAJI WA KUKU. 


Leo twende hatua sawa katika somo muhimu sana kuhusu ufugaji wa kuku. Ukiyafahamu haya basi utaweza kuvuka vipindi tofauti tofauti katika safari ya ufugaji wa kuku. Kabla hatujaendelea na somo naomba tumwagilie moyo kidogo maana haya maisha bila kumwagilia moyo unaweza kuwa unatembelea tovuti hii mara kwa mara ili uimarike zaidi kuhusu ufugaji.

Na kama ulikuwa haufahamu hizi nyakati katika shughuli ya ufugaji wa kuku basi twende bega kwa jino mwanzo mpaka maka.

Hizi nyakati nitazigawa katika makundi 7 kwa kuzipa herufi yaani A - G.

Tuanzie hapa maana kule kwingine wanafuga majoka.

A. Hapa unakuwa ni mtu ambae pengine hauna lengo la kufuga kuku lakini, inafika kipindi wazo la kufuga linakujia kichwani na wakati huo unashuhudia watu/ majirani wananufaika sana na ufugaji wa kuku pengine wanajenga , kununua usafiri au hata kusomesha. Sasa na wewe unakuwa na shauku kubwa sana kuhusu ufugaji wa kuku yaani unanunua mpaka vitabu, unatutafuta kina Lugalo Animal Care Platform kwaajili ya elimu za awali kuhusu ufugaji wa kuku. Katika kipindi hiki kuna vitu vinakusukuma miongoni ni hivyo tumevitaja hapo juu.

B. Hapa unaamua kuchukua hatua sasa ukiwa na mentality ya kuwa "nikiwa nawaza tu kuhusu ufugaji halafu sifugi ni sawa na kufugia kichwani" unaamua Kutafuta vifaranga pengine inawezekana usishirikiane na kina sisi ila unachukua kwa wazalishaji wengine. Unaweka oda na siku ya kuchukua vifaranga inafika na vifaranga kukufikia pengine utatumiwa au utavifata sehemu za kuzalishia....whatever. 

C. Vifaranga wanafika nyumbani yaani unapicha kubwa sana kupitia hao vifaranga. kawaida ya siku huwa hazirudi ila huwa zina songa mbele sasa kandri siku zinavo kuwa zinaenda kuna vijichangamoto huwa kawaida kuwepo kama vile vifaranga kufa na vyanzo visivyo bainika, kuwa unaishi tofauti na siku zote yaani pengine kuamka usiku ili kuangalia vifaranga na vikazi vidogo vidogo kama vile kubadilsha matandiko, usafi wa banda na vyombo nk...

D. Sasa hapa kuku walisha kuwa wakubwa na mziki ndipo unaanza. Utakuta gharama za chakula zimekuwa juu kwasababu wanaanza kula sana, magonjwa ndiyo usiseme yaani yanakuwa kama umeyafuga yapo bandani , kuna kiasi cha fedha ambacho kinahitajika kwaajili ya chanjo na madawa mbali mbali na chakula. Yaani katika kipindi hiki kinakuwa kigumu kiasi cha mfugaji kuona dhahili kuwa hapa sitoboi. Kale ka shauku kaliko kuwa kanakusukuma kule hatu A kanakusalti my friend...nakwambia pamoja na kutibu lakini wapi! piga Dua lakini wapi! piga Sara lakini wapi! inafika hatua unaanza kuwaza kuhusu hela uliyo chukulia vifaranga + hela ya chakula na madawa una assume kwamba nimeisha yaani mpaka unatufikiria kina Lugalo tunao kushauri bora tukalime miwa huenda tutanufaika na kazi yetu. 

katika hatua hii umekata tamaa lakini inawezekana kukawa na kitu ndani yako bado kinakuambia pamabana usife moyo ipo siku wako yaja _ameimba msanii_ 

E. Hatua hii wachache sana huwa wanaifikia kwa mujibu wa hayo mapito wengi huishia hatua D . Yaani hapa utakuta unauza kuku kwa bei ya hasara ilimradi tu waondoke au hauweki juhudi zozote kwaajili ya Kutafuta suluhisho. lakini kwa wasio wepesi wa kukata tamaa hatua hii wanaifikia yaani hawakati tamaa pamoja na kuwa changamoto zinawatinga sasa hapa unakuta pengine ulikuwa ni ugonjwa wa muda lakini wenye madhara kwa kasi. sasa itafika hatua kuku wataanza kujirejea wenyewe ikiwa nguvu ya juhudi zimekuwa za kawaida na ndiyo ukawa muda wa wewe kufahamu kuhusiana na kutengeneza chakula nyumbani yaani gharama za ufugaji zinapungua kwa kiasi chake, yaani unakuwa ni mtu wa kujisemea kumbe kila jambo linaufumbuzi wake hata kama siyo kibinadamu ila katika kila changamoto kuna Mungu ndani yake katika kuonyesha njia.

F. Hii ndiyo hatua ya kuelekea kileleni mwa ushindi yaani kama ni kuku wa mayai utakuta walisha anza kutaga kama ni kuku wanyama ulisha anza kuwauza yaani kiufupi upo kivurini una enjoy jux ft diamond kipindi hiki utakuta nyimbo za kusifu zinapigwa sana kwenye simu yako. Unasahua yale mapito ya hatua D. Na wakati mwingine unaweza kuta soko la mayai au nyama liko byee yaani ni mwendo wa ku collect vibunda tu na unakuwa na attitude za kibosi kweli kweli utasikia hello! Doctor ebu nitumie namba yako ya miamala niku bless ndugu yangu.

G. Hapa sasa ndipo tunapata mfugaji mzoefu ambae anaweza kushauri na wengine kuhusiana na ufugaji wa kuku kwani amepitia mengi sana kuhusu ufugaji wa kuku na katika hatua hii unakuwa huna wasiwasi kwasababu ulisha jua dawa wakaza za kutibu kuku, ulisha fahamu kuhusu wazalishaji wa vyakula wazuri yaani unakuwa na idea kubwa ya ufugaji wa kuku. lakini ungekimbia vita kule hatua D ungebaki kuwa mtu wa kuhadisiwa tu na kuona kwa wengine kuhusu faida za ufugaji wa kuku.

Lengo la makala hii ni kwamba katika ufugaji wa kuku kuna vipindi vigumu ambavyo unaweza kumbana navyo lakini isiwe tafsiri ya kuwa hakuna kitu unakifanya na hakuna kukata tamaa kwahiyo Yakupasa kuwa mvumilivu na maarifa amini hata hao unao waona wamefanikiwa kupitia ufugaji wa kuku haya mambo wanayapitia na walisha zoea yaani wapo hatua G.

Post a Comment

Previous Post Next Post