LEA VIFARANGA KWA UTARATIBU HUU....


BAADHI YA MAMBO MUHIMU KATIKA ULEAJI WA VIFARANGA, 

hapa tutangalia katika hatua ya upokeaji na uleaji wa vifaranga siku ya kwanza baada ya kufanya maadalizi kabla ya kupokea kama vile

1.kuandaa banda

2.kuandaa eneo la kulelea vifaranga ( bruda au kinengunengu )

3. kuweka matandiko

SASA TUONE MAMBO MENGINE YA KUFANYA BAADA YA HAYO YOTE KUFANYIKA

mfugaji unapo pokea vifaranga unatakiwa kuvikagua na kuhakikisha vina ubora, visiwe na vimelea vya magonjwa yoyote, hapa hakikisha kuwa vifaranga wamepewa chanjo ya kwanza ya ugonjwa wa mahepe ( marek's disease ) 

ULEAJI WA VIFARANGA NDANI YA MASAA MAWILI

zingatia ya fuatayo baada ya kupokea vifaranga ndani ya masaa mawili

1.ondoa vifaranga kwenye kasha na uviweke kwenye chumba au kwenye bridal ilivyo andaliwa

2.andaa maji ya uvuguvugu na weka kokoto kwenye vyombo vya maji ili kuepuka vifaranga kulowa

3.changavya glucose na maji ya uvuguvugu ( kijiko kimoja cha chakula kwenye lita kumi za maji ) kama hakuna glucose tumia sukari kijiko kimoja cha chakula kwenye lita tano za maji

4. wape vifaranga mchanganyiko huo wa glucose au sukari na maji ya uvuguvugu pekee kwa muda wa masaa mawili na usiwape kitu chochote 

5. hakikisha vifaranga wote wamekunywa 

6. vifaranga wasipewe chakula kabla ya kunywa maji ya uvuguvugu wa kutosha

ULEAJI WA VIFARANGA BAADA YA MASAA MAWILI

baada ya masaa mawili kupita mwaga maji yenye mchanganyiko wa glucose au sukari

Changanya maji safi na vitamin (kiwango cha kuchanganya angalia kibandiko cha kibebeo cha hiyo vitamin ) jaza kwenye vyombo vya kunyweshea na baada ya bapo weka chakula cha kuanzia ( chick starter ) kisha wape vifaranga 

MAMBO UKIZIGATIA WAKATI WA KULEA VIFARANGA

waangalie vifaranga kwa ukaribu ili wasilowane maji pia hakikisha hakuna maji yanayo mwagika bandani, wape vifaranga vitamini kila siku kwa muda wa siku tano za mwanzo, pia hakikisha unaamka nyakati za usiku kuangalia tabia au hali ya vifaranga kwa mfano ulaji wao,kulaliana, uchangamfu,joto na mwaga zingatia kiwango cha joto kinacho hitajika kama ifuatavyo

wiki ya kwanza 35 nyuzi joto

wiki ya pili 32 nyuzi joto

wiki ya tatu 29 nyuzi joto

wiki ya nne 26 nyuzi joto

wiki tatu za mwanzo vifaranga wapewe joto bandani muda 

✓ vifaranga wakisogelea chanzo cha joto tambu kuwa joto nikidogo hivyo yapaswa kuongeza joto

✓ vifaranga wakikaa mbali na chanzo cha joto tambu kuwa joto ni kubwa hivyo yapaswa kupunguza joto

✓ vifaranga wakiwa wameka siyo mbali wala katibu yani mkao wa kawaida basi joto liko sawa

ANGALIZO

kama joto ni kali: vifaranga hudumaa, manyoya huota ratatibu hulaji wa chakula hupungua na likizidi huweza kusababisha vifo

kama kuna baridi husababisha homa ( nimonia ya kuku ) pia vifaranga hujikusanya pamoja na kukosa hewa na kutokea vifo

CHANJO NA DAWA MUHIMU KWA VIFARANGA MPAKA WAKIWA WAKUBWA

vifaranga wapewe chanjo kulingana na maelezo ya mtaalamu wa mifugo

RATIBA YA CHANJO

siku/umri..... 2-6

chanjo/dawa..... pullorum Trisulmycine

ugonjwa..... pullorum

njia ya kuchanja...... wape kwenye maji

siku ya...... 7 -12 

chanjo/dawa...... lasota

ugonjwa mdondi/ kideri ( newcastle )

njia ya kuchanja..... wape kwenye maji

siku ya......14

chanjo/dawa......gumboro vaccine

ugonjwa........ gumboro

njia ya kuchanja..... wape kwenye maji

siku ya..... 21

rudia lasota

siku ya.....28

rudia gumboro vaccine

siku ya.....35

chanjo......fowl pox

ugonjwa.....ndui

njia ya kuchanja...choma kwenye bawa

Miezi mitatu wape dawa ya minyoo mojawapo ni piperazine citrate kwa kuwawekea kwenye maji

ANGALIZO

chanjo ya minyoo irudiwe kila baada ya miezi mitatu

kila baada ya zoezi la chanjo kuku wapewe vitamini

maji yatakayo tumika kwenye chanjo yasiwe na krorini inashauriwa maji yachemshwe siku moja kabla ya chanjo ili kuondoa madini ya krorini.

MAGONJWA SUBUFU KWA VIFARANGA

1. mhoro mweupe

2.mhoro mwekundu

3. mafua

Post a Comment

Previous Post Next Post