KAMA BADO HAUJA FUGA KUKU SOMA HII...

 


MFUGAJI AMBAE HAUJAFUGA UTAANZAJE KUFUGA?

Tuanzie hapa... 

Kikawadi linapo kuja swala la kuanzisha jambo fulani huwa kuna vipingamizi vingi sana, na vipingamizi hivyo ni pamoja na:

1. Hofu ( nitaweza kweli? )

2. Imani ( kuku wanafungwa na watu wenye kipato kikubwa)

3. Muda ( nani atanisaidia katika uangalizi kwani mimi kuna sehemu ambayo nahitajika kila siku za wiki na sina uwezo wa kuajili mtu )

4. Kugailisha ( ngoja nijipange ikifika mwezi fulani nitaanza )

Hivyo ni baadhi ya vipingamizi vinavyo fanya watu baadhi kushindwa kuingia kwenye industry ya ufugaji.

Hivyo basi leo nakupa ABC muhimu kwa mtu anae taka kuanza kufuga.

Hapa tuna makundi mawili ya watu wanao taka kuanza ufugaji wa kuku.

1. Mtu mwenye kipato kikubwa ( huyu lengo lake aanze moja kwa moja kufuga kibiashara )

2. Mtu mwenye kipato kidogo ( huyu lengo lake aanze kidogo kidogo na faida yake ndiyo imfanye aingie sokoni zaidi )

Sasa basi pamoja na huo utofauti lakini kuna hizi Sehemu ambazo zipo wazi kabisa kuwa utahijika kuingia gharama, Sehemu hizo ni zipi?

a) banda la kuku ( makazi )

b) vyakula

c ) matibabu & chanjo

d ) kwa wengine atahitaji msaidizi ( labda yeye ni mfanyakazi na watoto wapo shuleni )

e ) miongozo / elimu & mtaalamu. japo wafugaji wengi hili huwa hawaliweki kweny bajeti matokeo yake wanakutana na vitu ambavyo hawajui waanzie wapi? 

e) dharula ( emergency ) kwa mfano. Vifaranga wapo Sehemu ya kulelewa kinengunengu/ brooder , hapa utahijika kuwa na vyanzo vingine vya joto tofauti na umeme ( jiko la mkaa au taa ya chemli )

Kwahiyo wewe chakufanya hapa ili upate gharama kwa kila hicho kipengere ni kazi yako kuingia kwenye field ( uliza wanao fuga . Uliza wataalamu wa mifugo ) 

nikusaidie kidogo.

Viwango vya ulishaji wa kuku vilivyo fanyiwa tafiti ambavyo vipo kwenye nadharia vipo na mtu anaweza kukuchanganulia na mwisho wa siku mkapata makadilio ya jumla ya gharama kabla haujaanza safari ya ufugaji.

kwa mfano: tuwagawe hawa kuku kwenye makundi yao kulinga na uhitaji

1. Starter ( vifaranga maana yake watahitaji chakula cha starter )

2. Grower ( " " )

3. Layers ( " " )

sasa basi katika hayo makundi unatakiwa kufahamu:

vifaranga wa wiki la 1 hadi wiki la 8 watakula kiasi gani ndani ya huo muda wa kipindi cha kuwa lisha *starter* 

Hivyo hivyo na hayo makundi mengine ( grower na layers ) hayo ndiyo maswali unayo hitaji kwenda nayo kwa mtaalamu au mtu mwenye uzoefu katika ufugaji wa kuku.

Kwa upande wa banda hapo itategemeana na wewe unahitaji banda la namna gani pengine kuna banda uliliona sehemu fulani hivyo na wewe unataka kama lile kwahiyo itakuwa vizuri kwenda kuuliza gharama zake.

baada ya kupata bajeti pia kweny bajeti unatakiwa uwe na emergency kwani kuna vitu ambavy vinaweza tokea bila kukusudiwa, kwa mfano umeagiza vifaranga mara ikatokea unaambiwa kwa mkoa huo hatufanyi free delivery kwahiyo hapo itahitajika nauli.

kisha vifaranga wakisha fika huenda ukawa hauna miongozo maalumu ya kuwatunza vifaranga mara tu unapo wapokea hapa huenda ukawatafuta kina lugalo hapo napo utaambiawa miongozo ipo ila ina gharama sasa kwa kuwa wengi mnachukulia hizi kazi ni simple kwahiyo katika ile gharama unaona tunazingua 2 matoke yake unaamua kwenda kichwa kichwa. Wiki la 3 unarudi tena kuku wangu wanasinzia hapo utaambiwa kideri hatutibu ila huwa inatolewa chanjo na chanjo hutolewa siki ya 7 .

Tunaendelea.....

baada ya kukamilisha hayo yote na kuku wapo nyumbani kazi yako siyo kukaa kizembe yaan kuwa marafiki na wafugaji wazoefu ili wawe wanakupa dondoo wakaza kama vile changamoto kwenye upande wa vyakula , masoko bila kusahau kuwepo kweny magroup ya WhatsApp ya wafugaji na mara kwa mara kutembelea page za watu wanao toa elimu ya ufugaji wa kile unacho kifuga.

Wewe mfugaji kuna jambo unashindwa kwasababu upo mbali na watu sahihi kwako, jitafute kisha ujipate na ukisha jipata ingia kweny industry ya ufugaji.

Kama hapo ulipo unafuga kuku wa kienyeji basi ni mafanikio makubwa sana yatakayo kuwezesha kuaanza kufuga kibiashara , kuku ni walewale kwahiyo kufuga kuku wa kienyeji ni kufanya mazoezi ya kuanza kufuga kuku kibiashara.

Habari njema nikwamba formula za vyakula vya kuku ambazo zinafanya kazi na zinamatokeo mazuri tunazo, kwahiyo wewe na mtandao wetu wa kijamii ambao ni sifuri 673459117

Tunaendelea....

Alafu siyo lazima uanze na mazingira mazuri sana HAPANA! ila unaweza fanya hivi ili kupunguza gharama za ufugaji.

1. Vyombo vya chakula na maji ( utatumia ndoo / chonga ambazo hazina kazi ).

2. banda ( unaweza tumia jengo lisilo na kazi ukaliweka vizuri na kuezeka mabati au ukajenga bada la kawaida tu! )

3. Vyakula ( tafuta nafaka / mahitaji kisha andaa chakula chako mwenyewe kikubwa kuwa na msimamizi katika hili kama haujawa mzeofu )

4. Matibabu ( fanya usafi wa banda toa chanjo ili kuepuka matibabu / vifo )

5. Endelea kujifunza zaidi kukusu ufugaji.

Post a Comment

Previous Post Next Post