HIVI NDIVYO KUKU WAZAZI WANAVYO CHAGULIWA...

 


CHAGUA KUKU WA KUENDELEZA KIZAZI

Mafanikio zaidi katika kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi yatapatikana iwapo uchaguzi na uchambuzi wa kuku wanaozaliwa utafanywa mara kwa mara. Sababu kubwa ya kufanya uchaguzi ni kupata kundi la kuku litakalofaa kwa sifa zote katika uzalishaji. Sifa hizo ni pamoja na kupevuka haraka, kutaga mayai mengi, kuwa na uzito mkubwa na nyama nyingi kwa umri mdogo. Ufugaji bora utazingatia kuchagua kuku wenye sifa nzuri na kuwaacha waendelee na uzalishaji na wanaosalia wauzwe au waliwe.

Vilevile kuku wa Asili wanaweza kuboreshwa zaidi kwa kutumia majogoo ya kisasa kama vile Rhode Island Red-RIR ili kupata kuku wanaokua haraka wenye uzito mkubwa na kutaga mayai mengi zaidi

SIFA ZA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHAGUA MITETEA

Wawe na: 

-Umbile kubwa. 

-Uwezo wa kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 6). 

-Uwezo wa kustahimili magonjwa. 

-Uwezo wa kukua haraka. 

-Uwezo wa kutaga mayai mengi {zaidi ya 15 kwa mtago mmoja (clutch).

-Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi na kuwalea.

SIFA ZA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHAGUA MAJOGOO

-Jogoo bora, awe na:

-Umbo kubwa.

-Miguu imara na yenye nguvu.

-Kucha fupi. Mwenye nguvu. Machachari.

-Upanga/kilemba kikubwa.

-Uwezo wa kuitia chakula mitetea. 

-Tabia ya kupenda vifaranga

NJIA ZINAZOTUMIKA KATIKA KUCHAGUA KUKU WA KUENDELEZA KIZAZI

Kwa kuangalia kuku wenyewe kulingana na sifa zilizotajwa hapo juu. 

Kwa kufuatilia kumbukumbu za wazazi wa kuku unaotaka kuwachagua.

Kwa kuangalia kumbukumbu za familia (wazazi, kaka na dada).

WAKATI MUAFAKA WA KUCHAGUA KUKU WA KIZAZI ENDELEVU

-Mara tu wakitotolewa.

-Wakati wa ukuaji.

-Zoezi endelevu. Uzalishaji ukishuka chini ya asilimia 50. 

-Wakati kuku wanapoangusha manyoya.

FAIDA ZA KUONDOA KUKU WASIO FAA/ZALISHA KWENYE KUNDI

1. Inasaidia kuongeza uzalishaji wa mayai.

2. Inapunguza kulisha kuku ambao uzalishaji wake ni hafifu.

3. Inapunguza uenezaji wa magonjwa ya kuku.

4. Huongeza nafasi zaidi kwa kuku wazuri kwenye banda. 

5. Uwezekano wa kuuza kuku kama hao ni mkubwa kabla hawajafa.

UMRI WA KUKU KUPEVUKA

-Mitetea huanza kutaga wakiwa na umri wa miezi 6 - 8. 

-Jogoo huanza kupanda akiwa na umri wa miezi 7 lakini mbegu zake huwa bado kukomaa.

-Hutoa mbegu zilizokomaa anapofikia umri wa miezi 10.

Muhimu: Ni vizuri jogoo atumike kwa miaka mitatu tu ili kuepuka mchanganyiko wa damu kwa wenye nasaba moja kwani kufanya hivyo husababisha uzalishaji duni. Kama umeamua kufuga kuku wa mzao wa kwanza (F1) ni vyema kuwapandisha mitetea hao (F1) kwa majogoo ya asili ili kuendeleza damu ya asili.

UWIANO WA MATETEA NA MAJOGOO

Ili kudumisha amani katika kundi la kuku, na ili kupata mayai yenye mbegu ya jogoo ambayo yana uwezo wa kutoa vifaranga ni muhimu kuangalia uwiano kati ya mitetea na majogoo. Sio sahihi kuweka mitetea wengi kwa majogoo wachache na majogoo wengi kwa mitetea wachache. Uwiano unaokubalika ni wastani wa jogoo mmoja kwa mitetea kumi hadi kumi na mbili {1: 10-12}.

FUGA KUKU UPATE FAIDA KWA KUZINGATIA HAYA 

Elimu na Ushauri kutoka kwa mtaalamu wa mifugo na kutimiza yafutayo: 

1. Chanjo ya mdondo kila baada ya miezi 3. 

2. Chanjo ya ndui mara 2 kwa mwaka. 

3. Zuia viroboto, utitiri na minyoo. 

4. Chagua mayai bora kwa ajili ya kuatamiza. 

5. Panga kuuza kuku kwa makundi uongeze kipato. 

6. Boresha lishe ya familia kwa kula mayai na kuku. 

7. Gawa mapato yatokan

ayo na ufugaji wa kuku kwa matumizi yako (33%), maendeleo ya mradi (33%), na akiba (33%). 

Post a Comment

Previous Post Next Post