HAYA SIYO MAFUA...


 Leo ngoja tuangalie hili swala na ninaimani litakuwa muhimu sana kwetu sisi hasa wafugaji wa kuku, binafsi katika shughuli hii ya kufundisha wafugaji kuna mambo mengi sana na yafahamu.

Nikweli katika ufugaji wa kuku imeonekana ugonjwa wa mafua imekuwa tishio na kuwa kikwazo kwa baadhi ya wafugaji na wengine wanakata tamaa hasa pale wanapo kumbana na changamoto hii.

Sasa kwa kuwa ugonjwa wa mafua ndiyo  umekithiri sana matokeo yake kila dalili anayo onesha kuku basi wafugaji walio wengi moja kwa moja huamini ni mafua na kuchukua hatua za kutibu mafua.

Wengine hata hawaulizi ila wao wanacho amini ni mafua tu! lakini kwa upande mwingine ukija fatilia unakuta ni ugonjwa mwingine na wakati huo mfugaji ametibu huo ugonjwa kwa dawa za mafua bila mafanikio.

Na katika hili kuna vitu ambavyo wafugaji wanatakiwa kuvifahamu na muhimu zaidi ni kwenye dalili za magonjwa yaani mfugaji ukiona kuku anatoa undenda, macho kuvimba, kuwa na uteute mdomoni, kuwa na vitu kama povu jepesi la sabuni machoni na dalili zingine kama kushusha mabawa usichukulie kuwa hizo ni dalili za mafua na ukaanza kuchukua hatua za kutibu mafua bila kuuliza.

Hizo ni dalili ambazo zinaweza jitokeza katika magonjwa mengine tofauti na mafua na ugonjwa husika utabainika hasa pale utakapo shirikisha wataalamu au wafugaji wazoefu.

chakukushauri; ni kwamba kuku anapo umwa jitahidi kwanza kushirikisha wengine kabla hauja anza kuchukua hatua za kimatibabu.

Post a Comment

Previous Post Next Post