HAWA NDIYO BROILER...

  


KUKU WA NYAMA/BROILERS

Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku. 

Kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa NYAMA wamekua wakiuzika sana na Wanalipa Kibiashara kwa Wafugaji walioamua kuwekeza.

Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti.

Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo yameelezewa kama ifatavyo:-

CHAKULA 

Katika kuwalisha kuku matumizi ya chakula huweza kutofautiana kulingana na aina ya kuku pia na mazingira. Kwani kuna baadhi ya sababu ambazo zinaweza pelekea kuku kula sana au kula kidogo kwa mfano kuku wanaweza kula chakula kidogo ikiwa ni

1. joto

2. radha ya chakula

3. hali ya kiafya

Hizi ni miongoni mwa sababu chache ambazo zinaweza pelekea kuku kula chakula kidogo. lakini mbali na chakula pia wafugaji huwapa kuku:

1. Neoxychick &multivitamin siku 1-5

2. Vitamin kama Amintoto siku ya 7-10

3. Bro-booster na Mollases siku ya 11-24

4. Avipunch booster siku zilizo salia mpaka kuuza

N.B Matumizi hayo ya vitamin sio sheria , kutumika ili kupunguza gharama.

 CHANJO 

Kwa uzoefu wangu mfumo ambao nimezoea kuutumia

Siku ya 7 newcastle/kideri

Siku ya 14 Gumboro

Siku ya 21 Newcastle

Mfumo B

Newcastle siku ya 7

Gumboro siku ya 14

Gumboro siku ya 21

NB: Ndui haichanjwi kwa broiler, ila kwa wakati mwingine wamekua wakipata ndui iwapo watachelewa kuuzwa

 NAFASI

Kitaalamu broilers 10 wanafaa kukaa kwenye mita moja mraba, hii itasaidia sana kupunguza case za broiler kuchafuka kwa kulowesha maranda.

Kiasili broiler wanakunywa sana maji, hii hupelekea banda kuloana sana, hali hii imepelekea wafugaji wengi kuwa na kawaida ya kubadilisha randa Mara kwa Mara

Kubadili randa mara kwa Mara kwa mtazamo si sawa, ila unaweza ukawa unatoa palipo lowana sana na kubadilisha na randa kavu, hii itakusaidia sana kupunguza ugonjwa wa Mafua.

Nashauri kama itakua lazima sana basi randa zibadilishwe Mara 3 pekee IKIBIDI

MASOKO

Broiler wamekua wakiuzwa sana , kwa mtu mmoja mmoja, familia, supermarket, wauzaji wa nyama mitaani, mahoteli, mashule na sehemu kadha wa kadha NASHAURI tafuta soko lako la uhakika na uwe tayali kulilinda bei za broiler zinatofautiana mkoa kwa mkoa.

 MFUMO WA UGUGAJI

Ili kuhakikisha soko lako linakua lakudumu na kuepuka kupoteza wateja nashauri

Kama una mtaji ya kuku 500, nivema ukaingiza kuku 250 wiki hili, kisha 250 baada ya wiki 2 hii itarahisisha mzunguko wa pesa ya mradi, USIFUGE Kuku 500 kisha ukakaanao siku 30 ukiuza ndo uweke wengine itakua ngumu sana kukuza mradi ( kutokana na research ndogo niliyofanya pindi nawatembelea wafugaji ).

Kama nyama nyingine nyeupe, broilers pia wanasaidia kuimarisha afya ya malaji, ila mfugaji jitahidi kuto tumia kiwango kikubwa cha madawa ambayo yanaweza yakamdhuru mtumiaji wa mwisho

MAGONJWA KWA BROILER

Coccidiosis, kuhara ugoro au damu (dawa Agracox, vetacoxy, au Anticox kwa wanaohara damu)

Mafua , wahi mapema kubaini na unaweza kutumia ( Fluban, Flutan, Tylodox, na Enrovet)

Dawa hizi unapowapa wape na vitamin kupunguza stress kwao.

Post a Comment

Previous Post Next Post