HATA KANGA HUPATA MAGONJWA HAYA...

 


Kiwaida katika jamii za kiufugaji zinaamini kuwa kanga na kuku ni viumbe wawili tofauti na hawana uhusiano wowote, mitazamo hii hutokea hasa pale watu wanapo linganisha kanga na kuku katika kuathirika na magonjwa.

Ambapo inaonekana kuwa kanga mara nyingi huwa hathiriki na magonjwa na kufa kama ilivyo kasheshe kwa kuku, sasa kupitia vitu hivi ndiyo hupelekea watu baadhi Katika jamii kuamini kuwa kanga na kuku hawana uhusiano wowote.

Lakini tukija kitaalamu zaidi, kanga na kuku ni viumbe jamii moja na wana uhisiano mkubwa sana hasa kijenetiki na zaidi hawa wote ni jamii ya ndege, hivyo magonjwa mengi anayo athirika kuku hata kanga anaweza athirika vile vile.

ila utofauti unakuwa kwenye namna ya miili yao kanga ilivyo na uimara zidi ya kupambana na magonjwa, yaani hawa kanga miili yao hupambana na ina uimara zidi ya maambukizi ya magonjwa ndiyo maana mara zote huoneka ni ndege wasio pata magonjwa.

Hapa chini kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza athiri kuku na kanga;

Newcastle Disease: Hili ni tatizo kubwa kwa ndege wote na linaweza kusababisha vifo vya haraka.

Avian Influenza: Homa ya ndege inaweza kuwa hatari kwa aina zote za ndege.

Marek's Disease: Ugonjwa wa virusi unaoathiri mfumo wa neva wa kuku na pia unaweza kuathiri kanga.

Coccidiosis: Hiya ni maambukizi ya vimelea ambayo yanaweza kuwapata kuku na kanga.

Salmonellosis: Maambukizi ya bakteria ambayo yanaweza kuathiri mfumo wa utumbo wa ndege.

Post a Comment

Previous Post Next Post