FUNDISHA HAYA WASIMAMIZI WA MIFUGO WAKO...

 

Mfugaji elimisha na Kujifunza: Endelea kujifunza kuhusu mbinu mpya na za kisasa kuhusu ufugaji. Pia, elimisha wafanyakazi wako na familia kuhusu njia bora za kutunza mifugo ili kuongeza ufanisi wa ufugaji. Upo kwenye group unapata dondoo za ufugaji Alafu ukimaliza simu unaweka mfukoni na hauna mpango wa kuwa -subject watu wanao simamia mifugo wako nini unafanya sasa??? na hapa wengi ndipo mnafeli. tafuta elimu juu ya ulicho kifuga. Na unashauliwa kuwa na Elimu kabla ya kufuga.

japo wafugaji baadhi wanafuga kwanza kisha ndipo wanaanza mchakato wa Kutafuta Elimu juu ya walicho fuga. hili ni jambo ambalo linaweza pelekea mfugaji kukumbana na changamoto wakaza ambazo pengine haujui pakuanzia. Elimu juu ya unachotaka kufunga itakusaidia kuwa na A B C zidi ya hicho unachotaka kufunga hasa katika upande wa changamoto na faida/ masoko. Yaani hii 2024 mpaka iishe naamini kuna wafugaji mtaenda kufanya vizuri katika ufugaji wa kuku Kwani masomo tunayo kuandalia naweza sema ushindwe wewe tu.

Post a Comment

Previous Post Next Post