EBU FAHAMU HAYA KUHUSU DAWA...


 Katika ufugaji wa kuku linapo kuja swala la matumizi ya dawa hapa unatakiwa kuwa mtu mwenye kufata ushauri either ushauri wa wataalamu au wafugaji wazoefu ambao wanauzoefu katika matumizi ya dawa. 

jitahidi sana ukiwaanzishia dozi kuku wako basi hakikisha muda wa siku ya hiyo dozi unaisha, kumekuwa na mazoea katika matumizi ya dawa na nyuma yake kuna madhara japo siyo rahisi wewe mfugaji kufahamu hili.

Kwa mfano unaanzisha matibabu ya kuku ambayo yanatakiwa yaende mpaka siku 5 lakini wafugaji walio wengi huanza alafu baadae wanakatisha dozi, jambo ambalo ni hatari kwa mnyama wa aina yoyote hata kwa binadamu.

Wafugaji wengi hufanya haya ikiwa hawafahamu jinsi hizi dawa ambazo ni kemikali hufanya kazi katika mwili wa mnyama yaani wao hutamani kuku akipewa dawa leo basi kesho apone! jambo ambalo siyo rahisi kulingana na namna kemikali hizi zinafanya kazi katika miili ya viumbe.

Swala la dawa kusaidia mnyama kuwa katika hali nzuri ya kiafya ni mchakato kwahiyo kama ni mchakato basi yatupasa kuwa na subra.

Matumizi ya dawa tofauti tofauti katika muda usiyo sahihi ni hatari hasa katika afya na uzalishaji wa mifugo wako.

Kama dozi ni siku 5 basi nenda nayo kisha baada ya dozi kuisha subili angalau siku 3 ndiyo uanze kutumia dawa nyingine kama haujaona matokeo katika dawa ya awali. Huu ndiyo utaratibu mzuri katika swala la matumizi ya dawa na matibabu kiujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post