CHUNGUZA YAI KAMA LINA KIFARANGA...

 

NAMNA GANI NITAWEZA KUKAGUA MAENDELEO YA KIFARANGA KATIKA YAI

tutatumia neno candling likiwa na maana ya kukagua kifaranga ndani ya yai.

Candling ni sehemu muhimu sana katika ufugaji wa kuku hasa unapofanya uchunguzi wa ukuaji wa kifaranga ndani ya yai. Hivyo candling ya mayai inakusaidia kuona nini kinaendelea ndani ya yai katika kila hatua ya ukuaji wa kifaranga. Mwanga mulika yai kwenye eneo lenye giza unaweza kuona baadhi ya vitu ndani ya yai

Nini utaona wakati wa candling

Kwa yai hai lililorutubishwa utaona mishipa ya damu, kifaranga kikichezacheza na uwazi upande ule mkubwa.

Kwa yai ambalo kifaranga kimekufa (yai viza) huwezi kuona mishipa ya damu, utaona kifaranga ila hakichezichezi na huwezi kuona uwazi wa hewa upande mkubwa wa yai.

Kwa yai ambalo halikurutubishwa huwezi kuona chochote (mishipa ya damu, kifaranga).

Candling inatakiwa ifanyike kila siku hasa kwa wanaotumia mashine ili kubaini kama kuna tatizo lolote linalotokana na mashine na kulirekebisha. Chunguza yai moja baada ya jingine na hakikisha yai halikai nje ya incubeta zaidi ya nusu saa.

Candling ya mayai hatua kwa hatua

Hatua ya 1

Andaa eneo la giza kama unafanya candling wakati wa mchana hasa kwa utotoleshaji wa asili ukitegea kuku akiwa ameondoka kwenda kula. Tumia box au kitu chochote kutengeneza giza. Kwa utotoleshaji wa incubeta candling ni vizuri ikafanyika wakati wa usiku ambapo taa zitazimwa kuruhusu giza kuwepo.

Hatua ya 2:

Chukua yai moja moja kwa uangalifu kutoka kwenye kiota au incubeta na liweke upande mkubwa umulikwe na mwanga. Yaani upande mdogo uwe juu ( upande ulio chongoka ) na mkubwa chini unakotoka mwanga. Lishike yai upande ule mdogo kwa kidole gumba na kidole cha kati.

Hatua ya 3:

 Taratibu zungusha yai huku ukiliinamisha kidogo upande mmoja hadi pale unapoona vizuri.

Hatua ya 4

Tazama mayai kama yananyufa na mipasuko ili yaondolewe na weka alama eneo la hewa (uwazi upande ule mkubwa) ukitumia penseli zungusha mstari eneo hilo ili ikusaidie kulinganisha ukubwa kadiri siku zinavyoenda. Hatua ni pale unapofanya candling mwanzoni kabisa.

Hatua ya 5

Yape namba mayai kwa kutumia penseli tu wala si peni maana wino unaweza kupenya na kudhuru yai. Nayo hii inafanyika mwanzoni.

Hatua ya 6

Anza kufanya candling kila siku kuona maendeleo ya mayai. Toa yai na kurudisha kwenye incubeta au kiota kwa umakini ili usivunje. Hakikisha mikono yako ni misafi wakati wa candling. Andika matokeo ya candling kwa kila yai kwenye daftari la kumbukumbu.

MUHIMU

Unaweza kufanya candling kila siku tangu siku ya 1 hadi 16 au 17. Wengine hu candle siku ya 1, 7, 14 na 16.

Nini unapaswa kuona kwa siku unapofanya candling

Siku ya 1

Huwezi kuona chochote, japo candling siku ya kwanza ni muhimu ili kubaini kuwa mayai yote yanayowekwa kwenye incubator ni mazima, hayana mipasuko. Mipasukuko itaruhusu bakteria lakini pia kifaranga hakitatengenezwa, hivyo yasitumike.

Siku ya 4:

 Hapa utaona mishipa ya damu ikisambaa kwenye yai na itaonekana kama nywele. Kama hujaona chochote siku hii subiri siku ya saba kuna mayai mengine huchelewa kidogo.

Siku ya 7

Siku unatakiwa kuona mishipa ya damu vizuri na ule upande mkubwa utaanza kuona eneo la uwazi la hewa likijitokeza. Hewa hii itatumiwa na kifaranga.

Siku ya 10

 Hapa utaanza kuona kifaranga na kwa kiasi kinacheza cheza. Eneo la hewa sasa limetanuka na kuwa kubwa unaliona vizuri. Utaona pia kidoti cheusi kinachoonekana vizuri ambalo ni jicho la kifaranga. Hakikisha kufikia siku hii uwe ume kagua mayai yote.

Post a Comment

Previous Post Next Post