HILI SOMO LITAKUWEZESHA KUTENGENEZA CHAKULA CHA MIFUGO WAKO KIURAHISI HAPO NYUMBANI KWAKO.
katika somo la leo tutangalia namna ya kuweza kuchanganya vyakula vya mifugo mbali mbili pia kulingana na uhitaji wao, tambua kua zoezi la kuchanganya vyakula ni muhimu sana kwako wewe mfugaji kwani kufanya hivo utapunguza gharama za kununua vyakula madukani, hapa kinacho hitajika kwanza nielimu ya uchangaji wa vyakula vya mifugo, jabmbo jema hiyo elimu unaipata hapa kupita makala hii ya lugalo animal care, kitu kingine cha kuwa nacho ni marighafi,
✓ hakikisha chakula utakacho kipata baada ya mchanganyiko kina viini vifuatavyo
1. protini
2. wanga
3. madini
4 mafuta
5 na maji
MWISHO WA SOMO HILI UTAWEZA KUTENGENEZA CHAKULA CHA MAKUNDI YA WAVYAMA WAFUATAO
vifaranga nyama anza/broiler starter, vifaranga nyama kuzia, vifaranga mayai kuzia, chick mash, kuku mayai kuzia, kuku mayai taga, nguruwe watoto, nguruwe nenepesha, nguruwe kuzia, na ng'ombe wa maziwa,
Tuanzie hapa:
VIFARANGA VYAMA AZA
pumba 76kg
mashudu alizeti 15kg
dagaa sagwa 7kg
chokaa mifugo 0.5kg
premix 0.5kg
chumvi sagwa 0.5kg
VIFARANGA MAYAI ANZA
pumba 78kg
mashudu alizeti 16kg
dagaa sagwa 5kg
chokaa mifugo 2kg
premix 0.5kgkg
chumvi sagwa 0.5kg
NGURUWE WATOTO
pumba 76kg
mashudu alizeti 15kg
dagaa sagwa 6kg
chokaa mifugo 2kg
premix 0.5kg
chumvi sagwa 0.5kg
NGURUWE WA KUKUZA
pumba 76kg
mashudu alizeti 15kg
dagaa sagwa 4kg
premix 0.5kg
chumvi sagwa 0.5kg
NGURUWE NENEPESHA
pumba 80kg
mashudu alizeti 15kg
dagaa sagwa 2kg
chumvi sagwa 0.5kg
premix 0.5kg
KUKU MAYAI KUZIA
pumba 80kg
mashudu alizeti 12kg
dagaa sagwa 5kg
chokaa mifugo 2kg
premix 0.5kg
chumvi 0.5kg
KUKU MAYAI TAGA
pumba 80kg
mashudu alizeti 14kg
dagaa sagwa 3kg
chokaa mifugo 2kg
premix 0.5kg
chumvi sagwa 0.5kg
Kumbuka premix zina unzwa kwenye maduka ya bidhaa za mifugo, kwahiyo kama ulivyoona hapo juu kuwa premix imehusika katika kila mchanganyiko, na premix zipo za aina nyingi, mfano kama wewe unataka kutengeneza chakula cha kuku waliopo kwenye hatua ya kukua ( growers ) basi utanunua growers premix, kama ni kuku wanyama basi utanunua broiler premix, hivyo hivyo na kwenye Makundi mengine
pia sehemu yenye pumba unaweza gawanya mchanganyiko kwa mfano kama pumba inahitajika 80kg basi utachukua 20kg za mahindi palaza na 20kg za pumba pia kwenye chokaa utachukua nusu ya chokaa na nusu
na mifupa sagwa kwenye jumla ya kilo za choka zinazohitajika katka huo mchanganyiko.