BANDA BORA LA KUKU...

 


BANDA BORA LA KUKU 

Banda bora ni banda ambalo linakidhi mahitaji ya kuku wako na liendane na idadi ya kuku unaofuga.

Umuhimu wa banda bora

Banda bora linasaidia kupunguza changamoto za magonjwa

Sifa za banda bora.

I. Lijengwe sehemu isoyotuama maji 

II. Likinzane na uelekeo wa upepo na mvua 

III. Liruhusu mzunguko wa hewa

IV. Liwakinge kuku wako dhidi ya baridi 

V. Liwe na vichanja kwaajili ya kupumzika, kufanya mazoezi na kulala, pia Liwe na viota vya kutagia ambavyo huwekwa kuku wakifikisha miezi 3

VI. Liwe rahisi kusafishika

VII. Liendane na idadi ya kuku bandani

Hapa sasa watu wengi hua wanafeli na kujisababishia changamoto za magonjwa, kudonoana na kula mayai.

Kuku anahitaji sehemu ya kutosha ili aweze kuwa huru na kufanya mazoezi ndio maana wanaofuga huria au nusu ndani nusu nje wanapata matokeo mazuri. 

Kila aina ya kuku anahitaji nafasi yake.

1m square inahitaji kuku chotara 4/5 

1m square inahitaji kuku wa mayai 6/8

1m square inahitaji kuku wa kienyeji/nyama 8.

Mfano unataka kujenga banda la kuku chotara 100, unachukua 100÷4=25m square au 100÷5=20m square, sasa hii 25/20m square ndio ukubwa wa banda. 25=6.25x4 na 20=5x4.

Ukizingatia vipimo utapunguza changamoto. 

UMUHIMU WA VIOTA

Viota ni mahali ambapo kuku hutaga mayai, kuatamia na kuangua vifaranga. Hii inamaanisha kuwa viota ni sehemu muhimu sana ya kuzingatia ili kuweza kupata mayai mengi yaliyo salama pamoja na vifaranga.

Aina za viota

Kuna makundi mawili ya viota vinavyotumiwa na kuku pamoja na ndege wengine wafugwao.

1. Kiota kilicho tengenezwa na kuku mwenyewe

Hii ni aina ya viota ambavyo kuku huchagua mahali pa kutaga na kuhifadhi mayai. Inaweza kuwa mahali popote ambapo kuku ataona mayai hayataweza kudhurika au kuonekana. Kwa mfano, vichakani, stoo au kona yenye giza. 

Njia hii si nzuri kwani husababisha upotevu wa kuku na uharibifu wa mayai.

Kwa kutagia stoo au sehemu iliyojificha ya ndani, japokua ni sehemu salama ambayo haiwezi kufikiwa kirahisi na wezi au wanyama, mayai yanaweza kuharibika. Kuku akitaga sakafuni, sehemu yenye nailoni au magunia mayai yanaweza kuharibiwa na unyevu. Mayai hayo si mazuri kwa kutotoleshea. Itabidi mfugaji ayatumie au ayauze kwa ajili ya chakula.

Katika ufugaji wa ndani, kuku hutaga mayai sehemu yoyote hasa kipindi ambacho kuku huanza kutaga. Hii husababisha mfugaji kuyakanyaga mayai kwa bahati mbaya au kuku wenyewe kula mayai hayo na kupunguza uzalishaji wa mayai.

2. Kiota kilicho andaliwa na mfugaji

Kuku wanapotengenezewe viota vizuri huhatamia kwa utulivu kuongeza uzalishaji

Hii ni aina ya viota vilivyo andaliwa kiustadi na kuwekwa mahali stahiki kwa kumrahisishia kuku sehemu ya kutagia. Viota hivi huwekwa ndani ya banda au sehemu nyingine iliyoandaliwa. Viota vya aina hii huandaliwa kwa kuzingatia idadi ya kuku wanaotarajiwa kutaga, pamoja na upatikanaji wa vifaa vya kutengeneza viota.

MAHITAJI

Unaweza kutumia vifaa kama vile boksi la karatasi, mbao, nyasi, nguo aina ya pamba (isiwe ya tetroni), matofari na maranda. Boksi, tofali, na mbao husaidia kutengeneza umbo na ukubwa wa kiota. Nyasi maranda na nguo (viwe vikavu) husaidia katika uhifadhi wa mayai yasiharibiwe na unyevu, pia ni mazuri kipindi cha kuhatamia kwani hutunza joto.

Ukubwa wa kiota inategemea na umbo la kuku ukubwa wa kiota unatakiwa uwe ni wa kumwezesha kuku kuenea na kujigeuza. Hii ina maana kuwa unatakiwa uwe wastani wa sentimita 35 upana sentimita 35 au 30 na urefu sentimita 35.

ZINGATIA HAYA MFUGAJI 

Kiota kikiwa sehemu ya wazi ambapo kuku wengine ni rahisi kufika hawa kuku watamsumbua kuku anae atamia kwa kumpiga au hawa kuku wanaweza kula mayai.

Hivyo kiota kinatakiwa kiwe sehemu yenye mwanga hafifu

Sehemu ya kiota pakiwa pachafu panaweza kuwa na wadudu kama utitiri, viroboto wadudu hawa ni wasumbufu kwa kuku hivyo huweza kusababisha kuku atotoe Vifaranga vichache na mayai mengi kuharibika

Uwe na taratibu ya kuwachunguza kuku wanao taga au kuatamia, hasa hawa wanao atamia wafugaji wengi huwa hawana tabia ya kuchunguza maendelea ya afya zao. Hii inaweza sababisha kuku anae atamia kuumwa bila wewe kufahamu mwisho wa siku unakuta kuku kafa tu bila kujua ugonjwa ulimuanza lini

Kuku anae atamia apewe chakula na maji safi tena awekewe karibu na kiota chake ili asipoteze muda kwenda kujitafutia 

chakula, inaweza kuwa sababu ya kutotoa Vifaranga vichache na mayai kuharibika.


Post a Comment

Previous Post Next Post