TENGENEZA KINENGUNENGU HIVI ( BROODER )...

 


JINSI AMBAVYO UNAWEZA KUTENGENEZA KINENGUNENGU ( BROODER )

hiki ni kifaa cha kulelea vifaranga wakiwa wadogo.

1) Weka Kinengunengu ndani ya chumba cha kawaida kilichokuwa safi na chenye kupitisha hewa ya kutosha na wala sio chenye kupitisha upepo uvumao. 

2) Weka maranda, majani makavu yaliyokatwakatwa au makapi ya mpunga chini kwa ndani ya Kinengunengu. 

3) Tandika magazeti (makaratasi) juu ya maranda. 

4)Weka kifaa cha maji katikati ya Kinengunengu. 

5)Nyunyizia chakula cha vifaranga kiasi cha gao moja la mkono juu ya karatasi. 

6) Ingiza vifaranga wako ndani ya Kinengunengu huku ukiwahesabu. 

8) Fungua madirisha yote mawili ya Kinengunengu. Funika mfuniko wa juu wa Kinengunengu. 

Mambo ya kuzingatia unapotumia Kinengunengu

1) Vifaranga hukaa ndani ya Kinengunengu kwa muda wa kati ya siku saba hadi 14 bila kutolewa kutegemeana na mazingira pamoja na afya ya vifaranga vyenyewe. 

2) Joto linalotakiwa ndani ya Kinengunengu ni nyuzi joto kati ya 32 na 38. Iwapo mfugaji ana uwezo wa kununua kipima joto itamsaidia kupima na kurekebisha joto linapozidi au kupungua. 

3) Baada ya hapo weka uzio wa upana wa futi moja kuzunguka Kinengunengu kwa kutumia hardboard. 

4) Weka maranda ndani ya uzio uliozunguka Kinengunengu. 

5) Weka vyombo vya maji na chakula ndani ya uzio. 

6) Fungua milango yote minne iliyo chini pembezoni mwa Kinengunengu ili kuruhusu vifaranga vitoke nje kila asubuhi na kuvirudisha ndani ya Kinengunengu kila jioni hadi vifaranga vitakapofikia umri wa siku 28.

Kumbuka kwamba uzio unapanuliwa kila unapoona dalili ya vifaranga kubanana. Baada ya siku 28 hadi 42 vifaranga wanaweza kuachiwa ndani ya chumba chote

Faida za kifaa hiki

Kina uwezo wa kutunza vifaranga wengi kwa wakati mmoja.

Hupunguza vifo vya vifaranga kutokana na ndege na wanyama waharibifu mfano kunguru, mwewe, vicheche, karasa.

Kuku walionyang’anywa vifaranga vyao na kuvilea kwa msaada wa kifaa hiki, huweza kurudia kwenye mzunguko wa utagaji (wiki moja hadi wiki mbili) na kuweza kutotoa tena vifaranga kwa muda mfupi. 

Kifaa hiki hakina gharama ya nishati, na kwa zile sehemu ambazo zina baridi sana, basi huhitaji kiasi kidogo sana cha nishati

Vifaa vinavyotumika kutengeneza kifaa hiki ni rahisi sana na hupatikana sehemu zote nchini na gharama zake ni nafuu.

Post a Comment

Previous Post Next Post